Saturday, December 16, 2017

Uzinduzi wa Mradi wa Kinamama Mji MpyaNaibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. John Mnyika akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua mradi wa akina mama wa Mtaa wa Mji mpya Jimbo la Kibamba.

Mradi huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi  aliyoitoa Mhe. John Mnyika na Mwenyekiti wa Serikali ya  Mtaa Mhe. Aron Moye (kushoto kwa John Mnyika) wakati wakiomba ridhaa kwa wananchi.

Mhe John Mnyika na Mhe. Aron waliahidi kusaidia kuanzisha vikundi vya akinamama vya ujasiriamali.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi huo Mhe. John Mnyika aliwapongeza wakina mama hao kwa kuweza kutengeneza mfumo wa kusimamia mradi huo kabla haujaanza kwani miradi mingi imekufa kutokana na usimamizi.

Amewataka akina mama hao kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea.

Akitoa majibu ya changamoto zilizowasilisha Mhe. Mnyika aliahidi kufatilia ujenzi wa daraja kutoka Mji Mpya kueleka barabara kuu kupitia kwa Mangi na kumuelekeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kumpatia nakala ya maombi ya kupatiwa fedha kwaajili ya ujenzi huo aliyoiwasilisha Manispaa  kupitia kikao cha WDC ili kuweza  kuitengea fedha kwenye mfuko wa Jimbo.

No comments: