Sunday, January 3, 2010

Tanzania tumejiandaaje na soko la pamoja Afrika Mashariki linaloanza Julai 2010?

Leo nilikuwa live star tv kipindi cha "Tuongee Asubuhi" tukizungumza kuhusu uzalendo; mapenzi kwa taifa ama upendo wa watu wa nchi yetu. Niligusia hoja ya kwamba Novemba 2009 tumesaini itifaki ya soko la pamoja Afrika Mashariki na kwamba kuanzia Julai 2010 tutakuwa na mzunguko huru wa nguvu kazi, bidhaa na huduma(free movement of labour, goods and services).
Nilisema kwamba Kibaki kwa uzalendo wa nchi yake kwenye hotuba yake salam za mwaka mpya ameandaa wakenya kuchangamikia fursa hii na tayari walishaanza mageuzi ya kitaasisi kufikia azma hiyo. Lakini kwa Rais wetu Kikwete pamoja na kuwa alizungumzia mahusiano ya kimataifa kwenye hotuba yake, hakusema chochote cha kuwahamasisha watanzania kujipanga kwa changamoto zitakazojitokeza.
Nikaitaka Wizara ya Afrika Mashariki na Ikulu watoe tamko. Tanzania tumejiandaaje na soko la pamoja?

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Heshima kwako
Njia ya huku nimeiona kupitia ukurasa wako wa Facebook. Nimefurahi kusoma chambuzi zako na naamini kwa PAMOJA tutaweza kuinusuru na kuiendeleza Tanzania
Maoni ya bandiko hili nimeyaweka hukohuko Facebook
Pamoja Daima
Blessings