Wednesday, July 18, 2012

Mwito wa Polisi, Singida: Yanayojiri!

Nimefika Singida kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa Iramba kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Nimekutana na RPC, amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa kuwa kwa sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la tukio. Nimemuuliza RPC maswali mawili;

1. Wameniita kutoa maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?

Amenijibu kuwa ni mahojiano ya kawaida.

2. Kwanini mpaka sasa watuhumiwa 12 waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye mwanzo wa mkutano wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi wakiachia hali hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM hali ilitulia, Waitara akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name nikahutubia kwa amani na kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae mbali na tulipohutubia.

John John MNYIKA,

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)

18 Julai, 2012

1 comment:

Anonymous said...

Tunashukuru kwa ujulisho huo na tunasubiri more updates. Kuwa makini nao maana tumeshaambiwa unawindwa. Mwamini Mungu na kumtumainia naye atakushindia!