Thursday, April 3, 2014

TAARIFA KWA UMMA

Tangu tarehe 3/3/2014 Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Meck Sadiq ilipotoa tamko la kupiga marufuku biashara ya kusafirisha abiria maeneo ya mijini kwa kutumia usafiri wa bodaboda na bajaji kumekuwa na mgogoro baina ya vijana wanaofanya kazi hiyo kwa upande mmoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa upande mwingine.

Aidha, kufuatia kauli hiyo watumiaji wa kawaida wa pikipiki na bajaji nao wamekuwa wakipata usumbufu wa kukamatwa kamatwa na kusumbuliwa wakidhaniwa kwamba ni sehemu ya biashara ya usafiri kwa kutumia bodaboda na bajaji.

Kadhalika, kuanza tamko hilo limezusha usumbufu kwa abiria ambao walikuwa wakitumia vyombo hivyo vya usafiri kama mbadala wakati huu ambapo ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo kwa Haraka (BRT) imeambatana na ongezeko la foleni katika barabara zinazoelekea mjini.

Kwa upande mwingine pamekuwepo na utata kuhusu mipaka ya Eneo la Katikati ya Mji (Central Business District- CBD) linaloguswa na amri hiyo.

Kwa kuwa mwezi mmoja umepita bila mgogoro huo kupatiwa ufumbuzi na Serikali yenyewe, nimeamua kuingilia kati ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuwakilisha wananchi na kuisimamia Serikali.


Hata hivyo, kwa kuwa nipo katika Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba unaoendelea Dodoma ambapo sasa tupo katika hatua muhimu ya kupitia sura ya kwanza na sita za rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitaanza kwa hatua zifuatazo:

Mosi, nimemuandikia ujumbe mkuu wa Mkuu wa Mkoa Mecky Said kusitisha kwa muda utekelezaji wa tamko alilotoa ili kupisha mazungumzo baina ya Serikali, wahusika wa Bodaboda na Bajaji na wadau wengine muhimu ili kupata ufumbuzi.

Pili, Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ubungo 
Lengo la kuzuia vyombo hivi alisema ni kutokana kuongezeka kwa ajali pamoja na kushamiri kwa vitendo vya kihalifu hasa nyakati za usiku hivyo hakuna budi kudhibiti biashara hii, baadhi ya vitendo hivyo vihalifu ni pamoja na wizi unaofanywa na waendesha boda boda.

Tarehe 5/3/2014 Jumuiya ya Bodaboda na Bajaji wakiongozwa na viongozi wao wa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es salaam,walifanya mkutano mkubwa wenye lengo la kufanya tathmini juu ya kauli iliyotolewa na mkuu wa mkoa pamoja na kujadili hatua za kuchukua, ndipo walipofikia maamuzi ya kwenda ofisi za Sumatra.

Tarehe 8/3/2014 Viongozi wa Bodaboda na Bajaji walifika ofisi za Sumatra kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu kauli iliyotolewa na serikali ambapo walimkuta Mkurugenzi wa Barabara ambapo na yeye aliwaita maofisa wa biashara wa wilaya zote tatu ili kufanya majadiliano ya kina na viongozi wa Bodaboda na Bajaji.

Katika kikao hicho Viongozi wa Bodaboda na Bajaji walitaka kupatiwa ufafanuzi na Sumatra juu ya mipaka ya CBD yaani Central Business District inaanzia wapi na inaishia wapi ili kuweza kufahamu hayo maeneo ya mijini ambayo kwa mujibu wa tamko la mkuu wa mkoa hayaruhusiwi kufanya shughuli za kibiashara.

Hoja hii ilijibiwa na Mkurugenzi wa barabara katika ofisi za Sumatra nanukuu”baada ya kuanzishwa kwa CBD tayari imeshafanyiwa marekebisho mara mbili yaani marekebisho ya mwaka 1973 na mwaka 2009 ambayo yanatambua kua mipaka ya CBD inaanzia SAM NUJOMA-UBUNGO-TAZARA-AZIZ ALLY. kwa maana ya kwamba unaruhusiwa kubeba abiria kutoka mbezi mpaka ubungo ndio mwisho na kama utaingia ndani zaidi kwa maana ya manzese,magomeni,Lumumba basi utakua umevunja sheria hivyo ni halali kuchukuliwa hatua

Hata hivyo maelezo haya yanakinzana na maelezo yaliyotolewa na Halmashauri ya jiji ambapo kwa mujibu wa Halmashauri hiyo ni kwamba CBD ilianzishwa mwaka 1954 na inatambua kua mipaka inaanzia LUMUMBA-JAMHURI POSTA,hii inamaana kua Bodaboda na Bajaji wanaruhusiwa kubeba abiria mpaka eneo Lumumba lakini pia wanaruhusiwa kuingia mpaka postal.

Utofauti huu juu ya utambuzi wa mipaka kati ya Sumatra pamoja na Halmashauri ya jiji unapelekea Boda boda na Bajaji kuhisi kama wanaonewa na kuona kama sheria hii ni kandamizi isiyojali haki,hivyo kuamua kuchukua hatua zaidi kuona ni namna gani watapata haki yao.

No comments: