Sunday, September 26, 2010

Nikiwa na makamanda wa CHADEMA:Mdahalo wa Viongozi Vijana

Jumamosi, 25.09.2010 ilikuwa siku adhimu pale viongozi vijana na tumaini la Tanzania baadhi ya hazina ya CHADEMA tulioweza kuwakilisha tunu ya vijana makini wa CHADEMA katika mdahalo katika hoteli ya Movenpick. Mdahalo ambao ulikuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV ukiongozwa na Nguli wa Tansia ya Habari nchini, Jenerali Ulimwengu na Bibi Rose Mwakitwange.

Kupitia mdahalo huu, tuliweza kutanabaisha nini hasa tunu ya CHADEMA kwenu watanzania wote, na hivyo kuwapa fursa adhimu ya kuweza kufanya maamuzi mkiwa na taarifa kamili ya malengo yetu mema kwa Taifa letu na mustakabali wake.

Naamini, kwa waliopata fursa ya kuufatilia mdahalo-Hawatadanganyika!Watafanya maamuzi sahihi ya Kukichagua CHADEMA kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.


No comments: