Sunday, September 26, 2010

Jukwaa Moja na Kamanda Zitto!Mikutano yangu ya Mabibo

Wananchi waliweza kuona namna chama chetu cha CHADEMA kilivyo na ushirikiano mkubwa baada ya Kamanda Zitto Kabwe, Mgombea Ubunge Kigoma- Kaskazini alipoungana nami katika jukwaa moja kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kukipigia CHADEMA kura kuanzia madiwani wake, wagombea ubunge hususan John MNYIKA kwa jimbo la Ubungo na Mgombea wetu wa Urais, Dr.Slaa.Nikimnadi Mgombea Udiwani wangu, Kata ya Mabibo, Ndg. Msafiri. Wananchi wa kata za Ubungo naombeni mchague madiwani wa CHADEMA ili tuweze kufanya kazi nzuri katika halmashauri yetu. Hakika yale ya Tarime-Halmashauri kusomesha wanafunzi wa maeneo yao, ama huduma bora za kijamii katika Halmashauri ya Karatu yatawezekana tu Halmashauri za Jiji la Dar-es-Salaam endapo tutahakikisha madiwani wengi toka CHADEMA sambamba na wabunge wao wanashinda!


Moja ya jambo Kamanda Zitto alisisitiza; "Nipeni Mnyika tafadhalini sana tukafanye mambo mema kwa maslahi ya nchi hii, peke yangu ni kazi nzito sana. Wana wa Dar-es-Salaam kwa wajanja mpaka lini tutayakataa mabadiliko na kuendelea kutegemea watu wa mwisho wa reli Kigoma na wabunge wengine wengi wa vijijini kuwatetea?Tafadhalini sana mchagueni Mnyika, Chagueni madiwani wa CHADEMA wakafanye kazi ya kutetea maslahi ya Umma."


Tusake kura kwa kila mkazi wa Jimbo la Ubungo, Tupige Kura, Tuzilinde kura zetu, HAKIKA TUNASHINDA!!

1 comment:

Anonymous said...

hakika ntakupa Kura Kijana mwenzangu, mkazi wa mabibo