Sunday, September 26, 2010

Pamoja na Zitto; Mkutano wangu wa Kimara
Baada ya mkutano wangu wa Mabibo, tuliendesha mkutano mwingine Kimara. Nawashukuru sana wananchi wote mliojitokeza kwa wingi sana.Pia nawashukuru kwa namna ya kipekee kwa kuweza kuvunja rekodi ya uchangiaji katika mikutano yote kwa kuchanga papo hapo Tsh. 280,000/- za kuwawezesha mawakala siku ya kuhesabu kura Oktoba 31, 2010.

Vile vile nawashukuru wale wote ambao waliamua kujitolea Jenereta baada ya umeme kukatwa upande wetu "line yetu" tu katikati mwa hotuba yangu pale nilipokuwa naanza kuliongelea kwa kina suala la DECI!Mlithibitisha hawawezi kuzuia Nguvu ya Umma kwa kuweza kuleta mbadala wa Jenereta lenu wenyewe.
Viongozi wa Kichama wakifatilia hotuba ya John Mnyika, mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kwa UmakiniSehemu ndogo tu ya umati wa watu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa Kimara


Viongozi wa kichama pamoja na wananchi

3 comments:

Abner said...

Mh nakuamania na kukutakia kilala kheri katika michakato ya majukwaani sisi tuachie ya underground! Hongera kwa kazi nzuri!

Pjohn said...

that is a great campaign, i see what do u mean with this Country. We have a lot 2 do to this country.
In short i am studying with Steve (he works with u) at the UDSM.
The former MP did buy a lot of vans to sell water to ubungo peopele, it sucks a lot man,and i hate it. i feel like he is suppose to brought before the court of law for what he has done.
Pius John

nchemwa said...

kaka nakuombea kwa Mungu UFANIKIWE MAANA INAONESHA UNA MACHUNGUG YA KWELI NA NCHI HII.BIG UP.