Tuesday, September 21, 2010

Ratiba ya Kampeni Jimbo la Ubungo wiki hii 20Sept-26Sept

Ratiba ya Wiki hii itakuwa kama ifuatavyo;

Jumatano tarehe 22Sept-Mkutano wa ndani GOBA saa10 (0658242424),

Alhamisi 23Sept-Mikutano ya ndani KWEMBE saa9(0655583330) na KIBAMBA saa11(0718767749),

Ijumaa 24Sept-Mikutano ya hadhara MABIBO (0712802521) na KIMARA/SARANGA (0715393906),

Jumapili 26Sept -Mikutano ya ndani Sinza (0714061819) na UBUNGO (0754518597) na mkutano wa hadhara MAKUBURI (0718346811).

Wote mnakaribishwa kuhudhuria hasa wakazi wa maeneo yaliyotajwa.
**Tafadhali wasiliana na namba zilizotajwa kwa maelezo zaidi.

Tafuta Kura,Linda Kura,Piga Kura......Hakika Tunashinda!!!!

4 comments:

Anonymous said...

Kaka nimekupata na ratiba ya kampeni. Tupo nyuma yako daima. Sikuweza kuhudhuria mikutano yako ya siku za nyuma coz sikuwa na ratiba. Only today I have been able kutembelea blog yako na kuyaona hayo. Unafanya vizuri, unahitaji at least vijana kumi kila umapopita wa kiume watano na wa kike watano, ambao mara baada ya mikutano wawe wanapita kufanya kampeni za nyumba hadi nyumba wakiwashawishi wapiga kura kwa hoja kukichagua CHADEMA. Nimeona wananchi wengi wakielekezwa kwa namna hii wanaelewa hata wale waliokuwa wanasema ukinichanja damu yangu ni ya CCM wanabadilika ukikaa nao chini na kuwaeleza mfumo mzima wa uongozi na kwa nini tumefika hapa tulipo. Pata vijana wasomi wanaoelewa vizuri uongozi wa nchi yetu. Binafsi natumia nafasi niliyonayo kujaribu kuwaeleza watu hali halisi na nini CHADEMA inakusudia kufanya. Kaka nitakutafuta for more talk.

Anonymous said...

Daima nawe Kupata, kulinda na kupiga kura.

Anonymous said...

Kuwa na mikutano ya ndani ina umuhimu wake mkubwa kwani pale ndio mnajadiliana kwa kina kila jambo au matatizo yaliyo ndani ya eneo lako kwa umakini mkubwa.Pia kuna jamaa kapendekeza kuwa na vijana ambao watakuwa wanapita kuwaelezea watu umuhimu wa kuchagua CHADEMA nami naomba niongezee hapo kuwa wawe wanapita kuwashawishi watu hata hapo mkutano unapokuwa unaendelea kuna watu utakuta wanakaa nyuma kabisa kana kwamba hawapo hapo hawa wanahitaji mtu wa kuwahabarisha ilil kujua umuhimu wa kupiga kura kwa kuichagua CHADEMA.Hawa watasaidia kuwaelewesha watu sera na mikakati mbalimbali na umuhimu wa kuwa na madiwani wengi waq CHADEMA.Kila la kheri

Anonymous said...

NIMEKUKUBALI KINACHOTAKIWA KUWEKA USHINDI KABISA NI KUHAKIKISHA TUNAMROBBY MTIKILA ILI AWEZE KUKIUNGA MKONO CHADEMA KWA UHAKIKA TUNASHINDA