Monday, September 13, 2010

Mtaa kwa Mtaa, Kichochoro kwa kichochoro

Kuna wakati mwingine napenda sana kuwafata wananchi wangu katika maeneo yao haswa. Hapa natembea katika mazingira yao ya kila siku, yaani mitaani na vichochoroni kabisa. Nakatiza toka Magomeni Kagera ambako nilimaliza mkutano wangu wa hadhara kuelekea Mburahati.

Nashukuru sana wananchi ambao walikuwa wanajitokeza toka majumbani na kuja kunilaki!pia nawashukuru sana wale wote ambao waliungana nasi mpaka Mburahati ambako nilihutubia.
"Mheshimiwa kichochoro hiki kitatufikisha mapema na kwa urahisi zaidi"

Nilishuhudia wakina mama wakijitokeza na watoto wakiwa wamewabeba wakija kuniangalia na kunisabahi.Nawaomba kama mlivyojitokeza, tafadhali mjitokeze kwa wingi sana ninyi na marafiki zenu(shosti) wote katika kunipigia kura Oktoba 31, 2010.


Hawa walinipa hamasa na faraja sana pale walipoona msafara wangu unakuja kwa miguu waliponyoosha alama ya "V" alama ya CHADEMA!

3 comments:

Anonymous said...

kweli kaka mwanaume kugangamala, 2tafika

Filipo Lubua said...

Inshallah, Mungu atatufikisha. Pambana kaka.

Josephine said...

Eee Mola Muone mja wako