Saturday, September 11, 2010

Je unaniunga mkono kupata ushindi jimbo la Ubungo?

Ndugu,

Habari.

Je wewe ni shabiki, mwanachama, mfuasi ama mwananchi unayependa mabadiliko?

Je ungependa kushiriki katika safari ya kuhakikisha ushindi wa John MNYIKA katika jimbo la Ubungo?

Tafadhali naomba msaada wako wa kuungana nami katika kampeni za kimtandao kwa kuweka picha hii/poster ya “Namuunga mkono JOHN MNYIKA” kama "profile picture" katika facebook na twitter, pia tovuti na blogu kwa kadiri ya kipindi ambacho unajisikia unaweza kuweka kama sehemu ya mchango wako kwangu!


Nashukuru sana kwa baadhi ambao tayari wameiweka katika facebook!-msichoke, aluta continua.

NB: Kwa yeyote atakayepata shida ya kuiweka poster kama profile picture yake tafadhali usisite kuwasiliana nami;

johnmnyika@gmail.com au 0784-222222!


Inawezekana, Shiriki sasa!! Kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyatamani kuyaona.

3 comments:

suzie said...

Yaani JJ hii nayo unavunja mahusiano ya watu kabisa maana wengine hawaelewi, kwa mtazamo wangu kidogo inakuwa ngumu kuiweka kutokana na ukomavu wetu wengi katika siasa

josephine Edington said...

Ni kweli maana unaweza ukafikiria labda watu hawakusapoti ila ungeweka ya kwako na Dr. Slaa pamoja then uandike naisapoti CHADEMA at least, maana ni ngumu kifikra za watu wenye dhiki kutambua moja kwa moja kwamba ni kampeni tu. UBARIKIWE

MHANJO said...

USHAURI KUHUSU MKUTANO WA DR SLAA JUMANNE TARAKEA, ROMBO
Siku ya jumanne tarehe, 21/9/2010, DR SLAA, anatarajia kuhutubia wakazi wa tarakea, na kutumia uwanja wa shule ya secondary Tarakea, ambao uko zaid ya kilomita 3, kutoka tarakea mjini, tangazo hilo kuhusu mkutanao limetolewa na mgombea ubunge wa chadema , jimbo la ROMBO, JOSEPH SELASINI wakati akiwahutubia wakazi wa tarakea, leo saa kumi jioni.
Ushauri wa wapenda mabadiliko wilaya ya ROMBO wanawaomba chadema mtumie viwanja kati ya hivi viwili , cha kwanza ni stand ya bus tarakea, au cha shule ya msingi mbomai kati , ambacho kikokaribu na makazi ya watu na pia ndicho kilichotumiwa na jk, siku aliopokuja TARAKEA. Hivi viwanja viwili ni vizuri kwa sababu viko centre ya Tarakea, na ni rahisi kufikika na watu wengi, ukilinganisha na cha shule ya SECONDARY TARAKEA.
Natumaini viongozi wa chadema mtapata ujumbe , huu

Wapenda mabadiliko wilaya ya Rombo, mkoa wa Kilimanjaro

People power