Monday, July 26, 2010

Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo

MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika amepitishwa na na chama chake kugombea jimbo hilo kwa asilima 100.

Bw. Mnyika alipitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya wajumbe wote 62 kumpa kura ya ndiyo.

Wajumnbe waliohudhuria katika mkutano huo ni Wenyeviti na makatibu wote wa jimbo hilo, wageni waalikwa 60 na wawakilishi wa vyuo vikuu walioko Ubungo na wawakilishi wa matawi ya CHADEMA katika jimbo hilo.Wakati huo huo, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limemtaja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kuwa shujaa baada ya kukubalia maombi ya Kamati Kuu ya kugombea urais wakati baado alikuwa anahitajika katika jimbo lake.

Akizungumza katika mkutano wa wakilishi wa vyuo vikuu Mweyekiti wa Kamati ya baraza hilo, Bw. John Mnyika alisema kitendo alichofanya Dkt. Slaa cha kuachia jimbo ambalo alikuwa na uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ni la kishujaa.

"Tunakutana leo kwa kuwa tendo alilofanya Mtanzania mwenzetu, Dkt. Slaa kukubali kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la kishujaa," alisema Bw. Mnyika

Alisema Dkt. Slaa ni sawa mashujaa waliokubali kupoteza maisha yao na kulilinda na kuliteta taifa na hivyo ni shujaa wa demokarsia na maendeleo.

Alisema mashujaa wa namna ya Dkt. Slaa hawafii kwa kuwa fikra zao zitakumbukwa milele uamuzi wa huo utandika historia mpya kwa taifa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMA

Alisema Bendera ya chama hicho ni rangi ya nyekundu, nyeupe bluu, bahari na nyeusi uwepo kwa rangi nyekundu unatoka na kuthamini mashujaa wa nchi walipigana vita ili kulikomboa taifa hili.

Alisema maadhimisho yanayofanywa na serikali Julai 25 kila mwaka kuwakumbuka mashujaa ni unafiki kwa kuwa hufanywa kwa maneno na si wa kivitendo

Alisema tunu ya taifa hili ziko kwenye ngao ya taifa ambayo ni Uhuru na Umoja lakini uhuru umetoweka na nchi imekuwa tegemezi kwa kuwa sehemu kubwa ya rasilimli zake zimeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa wageni na sehenu kubwa ya Watanzania hawafaidi nayo

Alisema umoja umetelemshwa kutokana na kupuuzwa utawala wa sheria kumea kwa ubaguzi na kupanuka kwa matabaka katika jimii kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu na hata mifumo ya haki hali ambayo ni tishio la ustawi na usalama wa nchi.

Alisema Dkt. Slaa ametimiza wajibu huo kwa kusimamia ukweli, uwazi, uadilifu na amani kama rangi nyeupe katika bendera ya CHADEMA inayowakilishwa hususani kupitia ngazi ya ubungeni katika jamii na jimboni kwake karatu

Bw Mnyika alisema umefika wakati wa Dkt. Slaa kuinuliwa na kupewa wajibu mkuu zaidi katika nchi wa ili kuunda serikali na kusimamia utekelezaji ilikurudisha nchi kwa wananchi.

Chanzo: Gazeti la Majira 26/07/2010

No comments: