Tuesday, July 1, 2014

Maghembe awasilisha nyaraka za kuhusu Mnyika

Na Mary Geofrey

Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amepokea barua kutoka kwa Katibu wa Bunge ikimjulisha kwamba Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, hatimaye amewasilisha nyaraka na ripoti za utekelezaji wa miradi ya maji katika Jiji la Dar es Salaam.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu Msaidizi wa Mnyika, Aziz Himbuka, inasema kuwa taarifa hiyo imepelekwa katika Ofisi ya Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria wa Bunge ili iweze kusomwa na hatua zitakazohitajika zichukuliwe.

Alisema Mnyika ataanza kazi ya kuzipitia taarifa hizo katika Ofisi Kuu ya Bunge Dodoma na baada ya kazi hiyo atarejea kuanza ziara ya kikazi jimboni kwake kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu (Julai), 2014.

Mnyika anatarajia kufanya ziara katika kata zote 14, ambayo pamoja na mambo mengine atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya maji.Awali Mbunge huyo, alimtaka Waziri wa Maji, taasisi, mamlaka na kampuni zilizo chini ya Wizara ya Maji kumpatia nakala ya nyaraka zinazohusu masuala ya maji katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia masharti ya Sheria.

Chanzo: Gazeti la NIPASHE Julai 1, 2014 Ukurasa 3. (Toleo Na. 0578161 ISSN 0856-5414)

5 comments:

Unknown said...

Salam kwako Mhe, Mnyika.
Ni furaha kubwa kusikia unafatilia swala maji.
Jimbo linafahamika kwa kuwa na shida ya maji miaka yote.
Naomba nikukumbishe.
Wakati rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania , Mhe, JK akichaguliwa muhula wa kwanza ilitokana na kupendwa sana na raia Hasa vijana, tukiamini ni mchapa kazi na mengineyo, na wewe wakati tunakuchagua tulikuamini sana Hasa Sisi vijana kuwa utashughulikia kero muhimu za ki jamii, barabara na maji. Jimboni kwako na taifa kwa ujumla.
Sasa basi, kitaifa umejitahidi sana maana ni mmoja wapo uliyeibua madudu na yakafanyiwa kazi.
Ki Jimbo naona unapwaya kidogo. Ziara zako tangu tukuchaguwe ni kama hamna.
Tatizo la maji lipo pale pale tunanunuwa maji kwenye magari, na wakati huohuo serikali za mitaa maji yanatoka kwa wiki mara mbili, wanauza.
Foleni inayokuwa hapo ni mbaya sana. Wakati huo huo Yale mabomba yalitosambazwa yaki China yapo milangoni mwetu, na ndani ya fence. Kodi zetu zilitumika tukazika pesa, mabomba hayatowi maji ila serikali za mitaa yanatoka. Utajuaje haya kama hututenbelei.???.
Mhe, Mbunge. Barabara ndiyo usiseme tunaingia hasara kununuwa vipuri kila mara. Utadhani hakuna mbunge wala serikali.
Tangu tukuchaguwe Sina hata kumbukumbu greda lilipita lini kukwanguwa barabara. Jinsi shida ilivyo kwetu. Hebu niambie Mhe, unaweza nishawishi vipi nikuchaguwe tena muhula ujao??.
Sasa hivi ukianza kupita tunaona kama ni maandalizi ya kampeni.
Niwe wazi mimi ni mwanachama wako kwa siri,
Shida ninayoiona Ccm wakisimamisha mtu maili na mwenyewe sifa. Utakuwa wakati mgumu.
Hata kama usikilizwi kwa mambo ya Jimbo lako, ungetumia wakati mwingi kutembelea wananchi, ili uwape ukweli.
Jipange.
Naishi Mbezi kwa Msuguri, kata ya msigani,
Kero zipo hapa. Na dhani nakwingine zinafanana.

Anonymous said...

Julius Melkiory hujamtendea Mh. Mnyika haki. Mh. Mnyika ni kati ya wabunge wachache wasiokoma kufuatilia matatizo ya majimbo yao, iwe Bungeni au nje ya Bunge. Hajafanikiwa 100% kwa sababu yeye siyo mtendaji na kwa kweli hilo haliwezekani kwa sababu raslimali hazitoshi kufanya kila kitu. Mimi nampongeza na kumtaka akaze buti.

MKAZI WA MAKUBURI

Unknown said...

Juliad ni kweli kabisa Barabara ya kutoka kwa msuguli kwenda msigani na kwingineko ni kama vile serikali imetususia wananchi,kikubwa sisi wananchi tunalipa kodi stahiki mbaya zaidi barabara zingine zote grada limepita isipokuwa hii ya kwa msuguli kwenda msigani Mheshimiwa Mnyika tunakuamini na bajua grada kitapita kama segenu nyingine zote.

Anonymous said...

Muheshimiwa Mbunge , Tujuze ni lini hasa hizi barabara za mbezi mwisho to Masama mbeze beach, na ya goba to Tegeta, nyingine ya Malamba mawili mpaka kinyerezi zitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami, tumekuwa tukisikia hii kiini macho tangu 2011 ila hatuoni kinachooendelea, , Maji ndio kiini macho, Jimbo lako ni kero kero maji hakuna, pia kama alivyosema Julius, umekuwa busy na mambo ya kitaifa umesahau na jimbo lako sikumbuki ni lini nimekuona tangu nikuchague,

Anonymous said...

wabunge wa CHADEMA mnatakiwa kuwa makin kwn wenzen wa ccm kaz isha washnda.Nimeshangaa Kuona Matope Aliyo Fanya Mbunge Mwnye Eshma Bungen Anna Marechela Jmbon Kwake,kachimba Vcma Vya Maj Atuaa Mbili Nyuma Ya Chemchem Ya Maj Knachotoka Nitope2.....KAZENI BUTI CHADEMA 2015 NI YENU