Saturday, January 6, 2018
Saturday, December 16, 2017
Uzinduzi wa Mradi wa Kinamama Mji Mpya
Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. John Mnyika akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua mradi wa akina mama wa Mtaa wa Mji mpya Jimbo la Kibamba.
Mradi huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mhe. John Mnyika na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mhe. Aron Moye (kushoto kwa John Mnyika) wakati wakiomba ridhaa kwa wananchi.
Mhe John Mnyika na Mhe. Aron waliahidi kusaidia kuanzisha vikundi vya akinamama vya ujasiriamali.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi huo Mhe. John Mnyika aliwapongeza wakina mama hao kwa kuweza kutengeneza mfumo wa kusimamia mradi huo kabla haujaanza kwani miradi mingi imekufa kutokana na usimamizi.
Amewataka akina mama hao kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea.
Akitoa majibu ya changamoto zilizowasilisha Mhe. Mnyika aliahidi kufatilia ujenzi wa daraja kutoka Mji Mpya kueleka barabara kuu kupitia kwa Mangi na kumuelekeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kumpatia nakala ya maombi ya kupatiwa fedha kwaajili ya ujenzi huo aliyoiwasilisha Manispaa kupitia kikao cha WDC ili kuweza kuitengea fedha kwenye mfuko wa Jimbo.
Tuesday, December 5, 2017
Nasimama na Wabunge na Makamanda wetu waliokamatwa Morogoro
Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana.
Ikumbukwe walikamatwa toka Novemba 26 mpaka sasa wananyimwa haki yao ya msingi ya kupata dhamana.
Ninaheshimu mhimili wa Mahakama; lakini kwa yaliyowahi kwisha tokea na mifano lukuki inasukuma hitaji la sauti zetu. Kumeshakuwa na njama ovu nyingi dhidi yetu wapinzani hasa ktk suala zima la utoaji wa haki ya msingi ya dhamana-inahitaji kupazwa sauti zetu na kuunganisha nguvu kukemea hili.
Tuungane ktk hili na madhila mengine mengi ya uvunjifu wa haki, demokrasia na usawa ktk kuendesha siasa nchini.
Tunahitaji siasa safi ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama alivyotuasa Baba yetu, Mwl. Julius Nyerere
Thursday, August 3, 2017
MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI
MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri kivuli wa nishati na madini, Mhe. John Mnyika, akiongea katika Mkutano wa hadhara Jana Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, Mhe. Mnyika amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa nishati na madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.
"Ni muda mrefu umepita Rais ajateua Waziri wa nishati na madini, ambae ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya Katiba mpya" amesema Mnyika.
Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.
KATIBA MPYA
Mwaka 2010, akiwa Rais Kikwete, Mnyika ndiye aliyeibua mjadala kuhusu Katiba mpya ambapo ilipelekea hatua mpaka Rais Kikwete akaanzisha mchakato wa kipatikana Katiba mpya.
Mnyika ameahidi katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba 5 mwaka huu kuanzisha tena mjadala mpya utakaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho ya mambo mengi yanayoendelea.
KUHUSU MIRADI NA KERO JIMBONI
Katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu miradi na kero mbalimbali katika Jimbo, ambapo alisimama Mstahiki Meya wa Ubungo, Mhe. Boniface Jacob ambae alijibu maswali mbalimbali ya wananchi, pia kuwataka vijana na wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani kuna mikopo ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ujasiriamali na kujiendeleza katika mambo mbalimbali.
Na Sunday Urio
Katibu Msaidizi wa Mbunge, Jimbo la Kibamba
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri kivuli wa nishati na madini, Mhe. John Mnyika, akiongea katika Mkutano wa hadhara Jana Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, Mhe. Mnyika amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa nishati na madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.
"Ni muda mrefu umepita Rais ajateua Waziri wa nishati na madini, ambae ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya Katiba mpya" amesema Mnyika.
Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.
KATIBA MPYA
Mwaka 2010, akiwa Rais Kikwete, Mnyika ndiye aliyeibua mjadala kuhusu Katiba mpya ambapo ilipelekea hatua mpaka Rais Kikwete akaanzisha mchakato wa kipatikana Katiba mpya.
Mnyika ameahidi katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba 5 mwaka huu kuanzisha tena mjadala mpya utakaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho ya mambo mengi yanayoendelea.
KUHUSU MIRADI NA KERO JIMBONI
Katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu miradi na kero mbalimbali katika Jimbo, ambapo alisimama Mstahiki Meya wa Ubungo, Mhe. Boniface Jacob ambae alijibu maswali mbalimbali ya wananchi, pia kuwataka vijana na wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani kuna mikopo ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ujasiriamali na kujiendeleza katika mambo mbalimbali.
Na Sunday Urio
Katibu Msaidizi wa Mbunge, Jimbo la Kibamba
Monday, July 24, 2017
24 July: Ziara ya Ukaguzi wa Miradi katika Kata zote
Mbunge Wa jimbo la Kibamba Mh John John Mnyika leo tarehe 24/07/2017amefanya ziara ya kukagua miradi iliyofadhiliwa na Mfuko Wa Jimbo katika Kata zote sita zinazounda Ji mbo hilo ambazo ni Kata ya Saranga, Goba, Mbezi, Msigani, Kwembe na Kibamba.
Miradi hiyo ambayo ni vyoo vya Shule ya secondari Mpigimagohe , Kivuko cha Kibungobungo Kibamba, Ofisi ya Selikaliya mtaa Kinzudi Goba, Simtank Shule ya msingi msakuzi pamoja na fedha zilizoelekezwa kwenye vikundi vya ujasiliamali wanawake na vijana kwaajili ya kukuza mitaji yao.
Pia Mhe Mbunge aliwaagiza watumishi Wa Manispaa ya Ubungo kukamilisha miradi ambayo haijakamilika kwa wakati ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa kupitia fedha za mfuko huo.
Tuesday, July 18, 2017
Matengenezo ya haraka ya miundo mbinu-Kata ya Saranga
Jana Julai 17 Nilitembelea Kata ya Saranga na kujionea hali duni ya miundombinu ya barabara ambazo zimeharibika vibaya sana.
Kwa hatua ya awali nimekwishafanya mawasiliano na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo na Mkurugenzi wa Dawasco ili nao watembelee na kutuma watendaji kufanya matengenezo kwa haraka.
Nimetoa mwito, maeneo yote mabovu yawekwe kifusi lakini kwa hatua ya kudumu yawekwe slabu za zege kama ilivyofanyika kwenye baadhi ya maeneo kwenye barabara hiyo.
Muhimu:
Ziara ktk kata zingine tano ndani ya Jimbo letu la Kibamba zinakuja!
John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 18, 2017
Mazishi ya Mzee Mchungaji Mwasiwelwa
Jana, Julai 16 niliungana na wananchi wenzangu wa King'ong'o na kwingineko kumpumzisha Mzee wetu, Mch. Mwasiwelwa-Baba wa Mwenezi wetu, Perfect.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la milele. Aipe pia faraja na utulivu familia na wote ambao wameguswa na kuondokewa kwa Mzee wetu.
John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 18, 2017
Uzinduzi wa albamu mbili za Baraka Mwaijande katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni
![]() |
| Mkuu wa Jimbo, Mch.Mwangomola na Mchungaji wa Usharika wa Temboni, Mch.Lusekelo |
![]() |
| Baraka na Mkewe |
![]() |
| Kwaya ya vijana |
![]() |
| Nikiwa na Paul Clement |
Jumapili Julai 16: Nilibahatika kualikwa kushiriki uzinduzi
wa albamu mbili za kumsifu Mungu za kijana Baraka Mwaijande katika Kanisa la
KKKT Usharika wa Temboni , Jimbo la Magharibi-Dayosisi ya Mashariki na Pwani [ndani
ya Jimbo letu la Kibamba].
Nilifurahi na kufarijika sana kushuhudia vijana wakitumia vipaji vyao kumsifu Mungu.
Baraka pia alinigusa kiupekee sana kwa ndoto yake ya kujenga
kituo cha kuhudumia watoto yatima. Anafanya harambee kutekeleza azma hii.
Tumuunge mkono. Kwa wenye kutamani kusikia kazi zake mbili za kumsifu Mungu au
kumuunga mkono wawasiliane nae moja kwa moja: 0715-189 911
Paul Clement, alinigusa sana na wimbo wake “Amenifanyia Amani”!
Hakika ana kipaji cha kipekee.
Nimefurahi pia kuwa na Baba Wachungaji, Mkuu wa Jimbo-Mch.
Mwangomola, na Mkuu wa Usharika-Mch. Lusekelo na wachungaji wengine.
Naamini kila mmoja anaweza kuwa chachu ya kuiboresha jamii
yetu kwa kutumia vipaji/talanta tulizopewa na MUNGU vyema.
John John Mnyika,
Mbunge wa Kibamba,
Julai 17, 2017
Friday, June 30, 2017
MUHIMU: Nini maoni yako juu ya miswada iliyowasilishwa kwa hati ya dharura
MUHIMU:
Nawaomba wananchi wenye maoni/maboresho juu ya miswada (rasilimali+madini) iliyowasilishwa bungeni wanitumie kwa:
mbungekibamba@gmail.com
ISOME kupitia link hii: http://parliament.go.tz
John John Mnyika,
Waziri Kivuli-Nishati na Madini,
Mbunge wa Jimbo la Kibamba
Thursday, June 29, 2017
Monday, June 5, 2017
TANZIA: Mzee Philemon Ndesamburo
04 Juni, 2017: Niliweza kuwasili salama Moshi, KDC nyumbani kwa Mzee wetu Philemon Ndesamburo tayari kwa ajili ya shughuli ya kumpumzisha Mzee. Nikisaini kitabu cha maombolezo.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko jema la milele.
John John MNYIKA,
Mbunge-Jimbo la Kibamba,
Moshi, Juni 05, 2017
Friday, June 2, 2017
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA JOHN JOHN MNYIKA (MB), KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2016/2017 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/ 2018
(Inatolewa chini ya 99(9) ya kanuni za Bunge, Toleo la Mwaka, 2016)
- A. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Awali ya yote niungane na wenye mapenzi mema katika kuomba ulinzi wa mwenyezi Mungu wakati wa kutimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa Ibara ya 63 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuishauri na kuisimamia Serikali kwa Wizara ya Nishati na Madini juu ya bajeti ya mwaka 2016/2017 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, nitumie fursa hii kuwatakia waislamu wote mfungo mwema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mheshimiwa Spika, Nitambue mchango Mheshimiwa John Heche, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini alioutoa katika maandalizi ya hotuba hii. Aidha tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona na kurejea katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa pole kwa familia ya marehemu Mzee Philemon Ndesamburo, wanachama wa CHADEMA kote nchini, wananchi wa Moshi Mjini, wabunge na watanzania wote walioguswa na msiba huu. Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake kama mmoja wa waasisi wa chama chetu, Mbunge Mstaafu na Mfanyabiashara Mashuhuri. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema.
- B. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MUSTAKABALI WA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA
Mheshimiwa Spika, Novemba 4, 2016 Mheshimiwa Rais alipokuwa akizungumza na watanzania kupitia vyombo vya habari, ikulu jijini Dar es salaam alinukuliwa akisema hakuwahi kuzungumzia katiba mpya wakati wa kampeni zake, kwa hiyo siyo kipaumbele chake na kwamba anachotaka kwanza ni kunyoosha nchi.
Thursday, May 25, 2017
Kutoka Bungeni: Michango yangu mbalimbali
Swali kutoka kwa Mh Mnyika
Mnyika; swali kuhusu Maji Kimbamba
Source Simu.tv
Sunday, May 14, 2017
Mkutano wa hadhara wa Mmbunge wa Kibamba Mbezi Mwisho May 14
Wananchi na wabunge wao wakiwa kaatika maandamano ya kuangalia nyumba zilizochorwa alama nyekundu kwa ajili ya kubomolewa katika maeneo ya kuanzia Kimara, Mbezi hadi Kibamba. Maanadamano haayo yaliishia Kibanda cha Mkaa baada ya hali kuwa mbaya kwa msongamano wa magari
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiwafafanulia wananchi katika mkutano huo juu ya mipango ya barabara na sera za nchi juu ya mipaka
Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea akitoa neno kwenye tukio hilo
Mbunge wa Ubungo Said Kubenea na Mbunge wa Kibamba Mnyika wakiwa katika mkutano huo
Askari wa kikosi barabarani akimuomba Mnyika kupanda gari ili kuzuia wananchi wasiendelee kuleta msongamano barabarani
Wananchi wakimlalamikia trafiki baada ya kuamuru Mnyika kuondokaeneo hilo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo ya kawaida yaliishia hapo. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE,MO BLOG)
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiwafafanulia wananchi katika mkutano huo juu ya mipango ya barabara na sera za nchi juu ya mipaka
Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea akitoa neno kwenye tukio hilo
Mbunge wa Ubungo Said Kubenea na Mbunge wa Kibamba Mnyika wakiwa katika mkutano huo
Askari wa kikosi barabarani akimuomba Mnyika kupanda gari ili kuzuia wananchi wasiendelee kuleta msongamano barabarani
Wananchi wakimlalamikia trafiki baada ya kuamuru Mnyika kuondokaeneo hilo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo ya kawaida yaliishia hapo. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE,MO BLOG)
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika wa Jimbo la Kibamba na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wamejitokeza kwenye mkutano wa wazi uliofanyika jiioni ya leo eneo la Mbezi Mwisho ambapo wamesema wapo tayari kukaa meza moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Magufuli ili kuangalia utaratibu mwingine wa kuwaondoa wananchi ambao wanataakiwa kuondoka kupisha maeneo ya pembezoni mwa barabara ya Morogoro, ambapo wamepewa mwezi mmoja pekee kwa hatua hiyo amewataka wananchi waliokumbwa na zoezi hilo kujitokeza Mahakama Kuu ya Ardhi.
Kauli hizo zimetolewa leo na wabunge hao akiwemo Mbunge wa Kibamba, Mh. John Mnyika ambaye ameeleza kuwa, hapingani na Serikali, bali anataka haki itendeke kwa wananchi hao kwani wamepewa notisi ya mwezi mmoja tu na hawajajua fidia zao pia namna zoezi hilo likavyoathiri familia nyingi kwani wengine hadi sasa hawajui wataenda wapi.
“Narudia tena. Sipingani na maendeleo ya upanuzi wa barabara yetu. Ila tunaomba haki itende. Nawaombeni Madiwani andikeni barua ya kuonana na Rais pamoja na mie Mbunge wenu nitakuwepo kwenye hicho kikao. Tunahitaji haki. Kikubwa kwa sasa wananchi wote kesho asubuhi kuanzia saa mbili kwa wale waliowekewa alama ya kubomolewa tujitokeze kwa wingi Mahakama ya Ardhi kusimamisha zoezi hili kisheria” amesema Mnyika.
Hata hivyo baada ya kusema kauli hiyo na kufunga mkutano huo wa wazi, Mnyika alieleza kuwa, anataka kwenda kujionea maeneo hayo yaliyotiwa alama ya nyekundu ya X, ndipo kundi zima la wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kuungana na Wabunge hao naa kusababisha maandamano kwani wananchi wengi walijitokeza na kuunga msafara huo huku wakiimba nyimbo mbalimbalii walitembea kutoka sehemu hiyo ya Mkutano mpaka eneo la Kibanda cha Mkaa ambapo maandamano hayo yalisimama licha ya wananchi kuwa na hamu ya kutembea umbali mrefu ili kufikisha ujumbe wao.
Wananchi hao walikiwa wakisikika wakiimba “Tumechoka, Kubomolewa’ tumechoka kubomolewa” huku wengine wakiimba “Tanzania yetu sote, kwa nini tubomolewe” hata hivyo wakati Mnyika amewatuliza wananchi waishie hapo ili yeye aondoke kuendelea na majukumu yake baada ya Askari Polisi kueleza kwamba wananchi hao wanahatarisha usalama wa mambo mengine, Mnyika aliingia kwenye gari huku wananchi wakiwa na shahuku ya kulisukuma gari ilo, hata hivyo trafki aliamuru kuondoka mahala hapo na ndipo ukawa mwisho wa wananchi hao na kutawanyika
Mnyika ambaye pis ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kibamba awali katika mkutano huo alipokea kero mbalimbali huku kero kubwa ikiwa suala hilo la wananchi hao kuwekewa alama hizo nyekundu za kutakiwa kubomolewa pamoja na suala la Maji kwenye mabomba yao licha ya kuwekewa huduma ya mabomba.
Habari kutoka Mo Dewji Blog
Thursday, March 30, 2017
Ziara ya Kichama Mkoani Tanga
Tukiendelea na uimarishaji wa chama mkoani Tanga kwa mikutano na viongozi mbalimbali; kufanya tathmini na kupanga mikakati.
Tuesday, March 14, 2017
Tuesday, August 2, 2016
Kwaheri JOSEPH SENGA
Leo tumepata fursa kumuaga Ndugu yetu Joseph Senga.
Bado tunaendelea kumuombea kwa MUNGU amjalie pumziko jema la milele; kwa ubatizo alishiriki kuzaliwa upya nae basi kwa kifo ajaliwe kufufuka nae.
28 Julai 2016
UKUTA
1.0 UTANGULIZI
Kamati Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia tarehe 23-26 Julai, 2016 Jijini Dar Es Salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015. Mwenendo wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli, ni dhahiri kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidikteta katika nchi yetu.
2.0 MATUKIO MAHSUSI YA UKANDAMIZAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA NCHINI
2.1 Kupiga Marufuku Mikutano ya Vyama vya Siasa: Serikali kupitia Waziri Mkuu na hatimaye Rais na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuipa Serikali nafasi ya kufanya kazi. Huu ni uvunjaji wa Ibara ya 20 (1) ya Katiba. Aidha, katazo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya Vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi ya siasa.
2.2 Kupiga Marufuku Urushwaji wa moja kwa moja (live coverage) wa Mijadala ya Bunge: Katazo hilo ni kinyume na Katiba ibara ya 18 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa uhuru wa maoni na uhuru wa kupata habari kwa kila mwananchi.
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni: Serikali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb) ili kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe Serikali. Ikumbukwe kwamba Dkt. Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa; lakini ghafla anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM. Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais. Swali: Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Rais?
2.4 Kuingilia Mhimili wa Mahakama: Serikali ya CCM kupitia Rais, kwa nyakati tofauti imeonekana kujaribu kuingilia uhuru wa Mahakama jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini. Katika hotuba yake, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria duniani Rais alinukuliwa akisema kwamba Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu atatumia asilimia fulani ya fedha ambazo zitakuwa zimepatikana kutokana na faini za wale walioshindwa kesi kuwapa Mahakama.
2.5 Kupuuza Utawala wa Sheria: Tarehe 24 Juni, 2016 wakati wa uzinduzi wa siku ya usalama wa raia, Rais Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kuwapandisha vyeo watakaowauwa majambazi.
2.6 Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari –Serikali imepeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari. Sheria hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile kifungo cha miaka 15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu wa kifungu cha 6(6)
2.7 Serikali hii inatishia ukuaji wa uchumi Tangu serikali ilipoingia madarakani hali ya ukuaji wa uchumi na hata uwekezaji wa mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini mwetu na hata baadhi ya wawekezaji wanaondoa mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo unaoeleweka wa Kiuchumi.
2.8 Serikali za mitaa kunyanganywa mapato na serikali kuu. Baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda maeneo ya Majiji ya DSM, Mbeya,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa, Moshi,Bukoba,Babati,Tunduma na mingineyo ya maeneo ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia kodi ya Majengo Kodi ya Majengo inachangia kati ya 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.
2.9 Diplomasia na mahusiano ya kimataifa Hivi karibuni serikali imetoa maelekezo kupitia mawasiliano yake na Mabalozi (Note Verbale) kuelekeza kuwa kabla ya Mabalozi au maofisa wa Ubalozi kukutana na asasi zisizo za kiserikali au vyama vya siasa ni lazima kwanza waombe kibali cha serikali kupitia Wizara ya Mambo Nje. Utaratibu huu unaminya uhuru wa mabalozi na wanadiplomasia mbalimbali kufanya kazi zao nchini na ni utaratibu ambao unakiuka utamaduni uliokuwepo awali na pia unakiuka masharti ya Mkataba wa Vienna kuhusu mahusiano ya Kibalozi Duniani.
2.10 Uteuzi wa Wakurugenzi wa Halimashauri Uteuzi wa Rais wa Wakurugenzi wa Halimashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya haukuzingatia sheria za utumishi wa umma na badala yake umezingatia kigezo cha Ukada zaidi badala ya weledi na historia katika utumishi wa umma kama ambavyo sheria zinataka, zaidi ya wakurugenzi 80 na Makatibu tawala zaidi ya 40 waligombea kura za maoni ndani ya CCM 2015.
2.11 ZANZIBAR Kwa sababu ya hasira ya kukataliwa kwa CCM, vikosi vya ulinzi na hasa Jeshi la Polisi vimekuwa vikishiriki katika vitendo kadhaa vya ukiukwaji wa haki za raia huko Zanzibar ambapo kwa zaidi ya miezi miwili sasa, wamekuwa wakipita katika vijiji na kuwapiga, kuwatesa, kuwakamata, kuwatishia na hata kuharibu mali za wananchi na mifugo yao Tunawataka wananchi wa Unguja na Pemba waendelee kuikataa Serikali haramu iliyopo madarakani huko Zanzibar kwa njia za amani .
3.0 MAAZIMIO YA KAMATI KUU
Baada ya majadiliano Kamati Kuu imeazimia ifuatavyo;
3.1 Septemba 1, siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima Kamati kuu imeagiza ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi, Kata, Majimbo, Wilaya, Mikoa, Kanda, Mabaraza na Taifa kukaa vikao vyake vya kikatiba na imeelekeza ajenda ya vikao hivyo kuwa ni kujadili hali ya siasa, hali ya uchumi na maandalizi ya mikutano ya hadhara ya tarehe 01 Septemba, 2016 nchi nzima.
3.2 Wanasheria wa Chama kuchukua hatua Kamati Kuu imewataka wanasheria wa chama kukaa na kuyatazama mambo yote ambayo yametokea na kuchukua hatua za kisheria kwa lengo la kuyatafutia suluhisho la kisheria.
3.3 OPERESHENI UKUTA UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKTETA TANZANIA (UKUTA)
UTANGULIZI
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utangulizi kuna maneno yameandikwa na ambayo yamekaziwa na sheria namba 15 ya mwaka 1984 ibara ya 3 na sheria namba 1 ya mwaka 2005 ibara ya 3. Katika utangulizi huo wa katiba yetu imeandikwa kama ifuatayavyo;
“KWA KUWA Sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani”
“NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia, ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:” “KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa niaba ya Wananchi kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia ujamaa na isiyokuwa na Dini” Aidha kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana ibara ya 3 (1) inasema kuwa “Jamhuri ya Muungano ni Nchi ya Kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa” Ni wazi sasa kuwa kuna tishio kubwa dhidi ya ukuaji wa Demokrasia hapa Nchini mwetu kutoka kwa viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano kukandamiza Demokrasia na madhara ya kukandamizwa kwa demokrasia yameshaanza kulitafuna taifa letu. Ni dhahiri kuwa kama raia wema tuna wajibu na haki ya kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi na kuhakikisha kuwa haivunji na yeyote na misingi ya Kidemokrasia ambayo ilijengwa kwa miongo mingi inaendelea kuimarika, kulelewa na kukuzwa mara dufu.
3. 4 KWANINI UKUTA NI MUHIMU !
3. 4 KWANINI UKUTA NI MUHIMU !
Wakati wa Ufashisti wa Adolf Hitler huko Ujerumani unaanza kuchipua kabla ya kukomaa alianza kuchukua hatua mbalimbali za kuwanyamazisha Wajerumani kwa njia mbalimbali ili aweze kutawala kwa mkono wa Chuma. Alikuwepo Mchungaji mmoja anayejulikana kwa jina la Martin Niemoller na ambaye alikuwa akimsemea Hitler kwa kila hatua ambazo alikuwa anachukua dhidi ya makundi mengine katika jamii ya wajerumani bila kujua kuwa lilikuwa ni suala la muda tu kabla hata yeye hajafikiwa na mkono wa Chuma wa Hitler. Mchungaji huyu ni maarufu sana kwa msemo wake ambao aliutoa alipofikiwa na mkono wa Hitler ambao ulimpelekea kuishia jela kwa miaka 7 na wakati huo hapakuwa na mtetezi wa kumsemea, alisema hivi;
" First they came for the Socialists, and I did not speak out— Because I was not a Socialist.
Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out— Because I was not a Trade Unionist.
Then they came for the Jews, and I did not speak out— Because I was not a Jew.
Then they came for me—and there was no one left to speak for me."
3.5 HALI TANZANIA IKOJE?
3.5 HALI TANZANIA IKOJE?
Tangu utawala wa awamu ya Tano ulipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015 umechukua hatua mbalimbali za kubinya Demokrasia na kuua dhana ya utawala bora kwa njia mbalimbali.
Yapo makundi ya kijamii ambayo tayari yameshaumizwa au kubinywa na watanzania walio wengi wanakaa kimya kwa sababu wao sio sehemu ya kundi husika ambalo limenyimwa haki au kwa kuwa hajafikiwa moja kwa moja.
3.6 KWANINI NI MUHIMU KUJENGA UKUTA.
3.6 KWANINI NI MUHIMU KUJENGA UKUTA.
- Rais alipiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma- sikusema kwa kuwa mimi sikuwa mtumishi wa umma
- Rais aliitaka mahakama kuu iwahukumu wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi na serikali lazima ishinde-sikusema kwa kuwa sikuwa mfanyabiashara na wala sikuwa na kesi ya kodi
- Serikali iliingilia Bunge na kupanga kamati za kudumu za Bunge-sikusema kwa kuwa mimi sikuwa mjumbe
- Serikali ilizuia matangazo ya Bunge live-sikusema kwa kuwa mimi sio Mbunge
- Wabunge wa Upinzani kunyanyaswa Bungeni na kuonewa –sikusema kwa kuwa mimi sio UKAWA
- Hotuba za Upinzani kufutwa Bungeni kinyume cha Kanuni za Bunge –sikuwa mpinzani nilikaa kimya
- Bunge kurejesha fedha zake kwa Rais kinyume cha sheria –sikusema kwa kuwa halinihusu
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi kurejesha fedha kwa Rais kinyume cha sheria –sikusema kwa kuwa Tume hainihusu
- Serikali Kuwafukuza na kuwadhalilisha wanafunzi wa UDOM –sikusema kwa kuwa sina ndugu wala mtoto anayesoma UDOM.
- Mikutano ya kisiasa kupigwa Marufuku –sikusema kwa kuwa mimi sio mwanasiasa
- Wafanyabiashara kupelekewa bili kubwa za kodi na hata kuzuiliwa kwa Akaunti zao-sikusema kwa kuwa mimi sio mfanyabiashara
- Uchumi unaporomoka kwenye sekta zote nchini -sikusema kwa kuwa mimi sijawahi kumiliki uchumi
- Fao la kujitoa limeondolewa kwenye Mifuko ya hifadhi ya jamii, sikusema kwa sababu mimi si mwanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
- Mashirika na Makampuni kuanza kupunguza wafanyakazi kutokana na kuporomoka kwa uchumi –sikusema kwa kuwa sijapunguzwa kazini
- Mabalozi na wanadiplomasia kuzuiliwa kukutana na viongozi wa kisiasa bila kibali cha serikali- sikusema kwa kuwa halinihusu
- Watumishi wa umma kulazimishwa kwenda kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma wametakiwa kuwa Makada wa CCM –sikusema kwa kuwa mimi sio mtumishi wa umma
- Ukaguzi wa vyeti vya kidato cha nne na kutumika kama msingi wa kufukuza watu kazi hata kama ni Maprofesa –sikusema kwa kuwa hawajaja kwenye sekta yangu
- Watumishi wa umma kutumbuliwa majipu bila kufuatwa kwa sheria na kanuni za utumishi wa umma –sikusema kwa kuwa mimi sikutumbuliwa
- Mawakili kuunganishwa kwenye kesi za wateja wao wanapoenda kuwatetea –sikusema kwa kuwa mimi sio wakili
- Waalimu kukatwa mishahara iwapo dawati litavunjika kwenye shule yake –sikusema kwa kuwa mimi sio mwalimu
- Kupotezwa kwa wana CCM ambao watapinga kauli ya Mwenyekiti au kuwa na maoni tofauti-sikusema kwa kuwa mimi sio mjumbe wa vikao vya CCM .
- Muswada wa sheria ya haki ya kupata habari na adhabu ya kifungo cha miaka 15-20- sikusema kwa kuwa mimi sio mwandishi wa habari
- Viongozi wa dini kudhalilishwa –sikusema kwa kuwa mimi sio kiongozi wa dini
- Unyanyasaji na udhalilishaji wa wananchi Zanzibar –sikusema kwa kuwa mimi sio mzanzibari
3.7 TUCHUKUE HATUA!
i. Kwa kuwa wewe tayari umeshafikiwa hauna budi kujenga UKUTA ili kuzuia wengine wasidhurike na utawala huu.
ii. Kwa kuwa wewe hujafikiwa na ndio maana husemi wenzako wanapofikiwa, njoo tujenge UKUTA ili ukifikiwa awepo wa kusema
iii. Tuungane Tujenge UKUTA ili kuzuia uchumi wetu kuporomoka
iv. Njoo Tujenge UKUTA kuzuia Udikteta huu
v. Tujenge UKUTA tuilinde Katiba yetu
vi. UKUTA huu ni wa wananchi wote bila kujali dini, kabila, chama cha siasa au rangi
Historia inaonyesha kuwa Duniani pote Hakuna utawala uliwahi kuushinda UKUTA wa wananchi .Na hii ndio Nguvu ya Umma. Kila mmoja achukue hatua popote alipo ya kujenga UKUTA!
Imetolewa na
Freeman A Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
27 Julai, 2016
Imetolewa na
Freeman A Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
27 Julai, 2016













































