Thursday, September 30, 2010

Nikiwa na wananchi Goba!!






Kamanda Gwanda Kilewo akiongea na kuhamasisha wananchi wachague safu ya CHADEMA Oktoba 31, kuanzia Mgombea Udiwani, Mbunge MNYIKA na Rais Slaa!

Nikiwa na Diwani wangu Mushi, Diwani wa Goba anayesubiri Kuapishwa!!

Diwani Mushi, Diwani wa Kata ya Goba. Hakikisheni mnanichagulia safu ya madiwani wangu tuweze kusafisha uozo katika Halmashauri ya Kinondoni

CHADEMA inathamini sana mchango wa makamanda wanawake, hapa Kamanda Judith KAPINGA akiongea na wananchi, pembeni Kamanda Makwilo


Kamanda Edward Kinabo akielimisha, hamasisha wananchi kupigia kura CHADEMA ngazi zote Udiwani-Ndg Mushi, Ubunge-MNYIKA, na Urais-Dr.Slaa

Monday, September 27, 2010

MWANANCHI 27.09.2010 MNYIKA KATIKA KAMPENI NA ZITTO

Nashukuru sana vyombo vya habari vyote ambavyo vinaendelea kuwa mstari wa mbele kuripoti taarifa za mikutano na kampeni zangu kwa ujumla. Vipo vyombo vya TV, Radio, blogu, magazeti. Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mkubwa mnaoutoa-hakika mnatoa mchango mkubwa sana si tu kwangu na kampeni bali kwa ukuaji na ukomavu wa demokrasia nchini mwetu.

Aluta Continua, Maslahi ya Umma Kwanza!

Sunday, September 26, 2010

Nikiwa na makamanda wa CHADEMA:Mdahalo wa Viongozi Vijana

Jumamosi, 25.09.2010 ilikuwa siku adhimu pale viongozi vijana na tumaini la Tanzania baadhi ya hazina ya CHADEMA tulioweza kuwakilisha tunu ya vijana makini wa CHADEMA katika mdahalo katika hoteli ya Movenpick. Mdahalo ambao ulikuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV ukiongozwa na Nguli wa Tansia ya Habari nchini, Jenerali Ulimwengu na Bibi Rose Mwakitwange.

Kupitia mdahalo huu, tuliweza kutanabaisha nini hasa tunu ya CHADEMA kwenu watanzania wote, na hivyo kuwapa fursa adhimu ya kuweza kufanya maamuzi mkiwa na taarifa kamili ya malengo yetu mema kwa Taifa letu na mustakabali wake.

Naamini, kwa waliopata fursa ya kuufatilia mdahalo-Hawatadanganyika!Watafanya maamuzi sahihi ya Kukichagua CHADEMA kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.


Pamoja na Zitto; Mkutano wangu wa Kimara




Baada ya mkutano wangu wa Mabibo, tuliendesha mkutano mwingine Kimara. Nawashukuru sana wananchi wote mliojitokeza kwa wingi sana.Pia nawashukuru kwa namna ya kipekee kwa kuweza kuvunja rekodi ya uchangiaji katika mikutano yote kwa kuchanga papo hapo Tsh. 280,000/- za kuwawezesha mawakala siku ya kuhesabu kura Oktoba 31, 2010.

Vile vile nawashukuru wale wote ambao waliamua kujitolea Jenereta baada ya umeme kukatwa upande wetu "line yetu" tu katikati mwa hotuba yangu pale nilipokuwa naanza kuliongelea kwa kina suala la DECI!Mlithibitisha hawawezi kuzuia Nguvu ya Umma kwa kuweza kuleta mbadala wa Jenereta lenu wenyewe.
Viongozi wa Kichama wakifatilia hotuba ya John Mnyika, mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kwa Umakini



Sehemu ndogo tu ya umati wa watu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa Kimara


Viongozi wa kichama pamoja na wananchi

Jukwaa Moja na Kamanda Zitto!Mikutano yangu ya Mabibo

Wananchi waliweza kuona namna chama chetu cha CHADEMA kilivyo na ushirikiano mkubwa baada ya Kamanda Zitto Kabwe, Mgombea Ubunge Kigoma- Kaskazini alipoungana nami katika jukwaa moja kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kukipigia CHADEMA kura kuanzia madiwani wake, wagombea ubunge hususan John MNYIKA kwa jimbo la Ubungo na Mgombea wetu wa Urais, Dr.Slaa.



Nikimnadi Mgombea Udiwani wangu, Kata ya Mabibo, Ndg. Msafiri. Wananchi wa kata za Ubungo naombeni mchague madiwani wa CHADEMA ili tuweze kufanya kazi nzuri katika halmashauri yetu. Hakika yale ya Tarime-Halmashauri kusomesha wanafunzi wa maeneo yao, ama huduma bora za kijamii katika Halmashauri ya Karatu yatawezekana tu Halmashauri za Jiji la Dar-es-Salaam endapo tutahakikisha madiwani wengi toka CHADEMA sambamba na wabunge wao wanashinda!


Moja ya jambo Kamanda Zitto alisisitiza; "Nipeni Mnyika tafadhalini sana tukafanye mambo mema kwa maslahi ya nchi hii, peke yangu ni kazi nzito sana. Wana wa Dar-es-Salaam kwa wajanja mpaka lini tutayakataa mabadiliko na kuendelea kutegemea watu wa mwisho wa reli Kigoma na wabunge wengine wengi wa vijijini kuwatetea?Tafadhalini sana mchagueni Mnyika, Chagueni madiwani wa CHADEMA wakafanye kazi ya kutetea maslahi ya Umma."


Tusake kura kwa kila mkazi wa Jimbo la Ubungo, Tupige Kura, Tuzilinde kura zetu, HAKIKA TUNASHINDA!!

Thursday, September 23, 2010

MABIBO NA KIMARA LEO 24Sept

Mikutano ya hadhara miwili ya leo itahutubiwa na Mhe Zitto Kabwe ...Karibu sana!!

1.MABIBO Mpakani saa 9-10 Jioni

2.KIMARA Stendi saa 11-12 Jioni

Usikose

Tafuta Kura ,Piga Kura ,Linda Kura....Hakika Tunashinda!!

Tuesday, September 21, 2010

Ratiba ya Kampeni Jimbo la Ubungo wiki hii 20Sept-26Sept

Ratiba ya Wiki hii itakuwa kama ifuatavyo;

Jumatano tarehe 22Sept-Mkutano wa ndani GOBA saa10 (0658242424),

Alhamisi 23Sept-Mikutano ya ndani KWEMBE saa9(0655583330) na KIBAMBA saa11(0718767749),

Ijumaa 24Sept-Mikutano ya hadhara MABIBO (0712802521) na KIMARA/SARANGA (0715393906),

Jumapili 26Sept -Mikutano ya ndani Sinza (0714061819) na UBUNGO (0754518597) na mkutano wa hadhara MAKUBURI (0718346811).

Wote mnakaribishwa kuhudhuria hasa wakazi wa maeneo yaliyotajwa.
**Tafadhali wasiliana na namba zilizotajwa kwa maelezo zaidi.

Tafuta Kura,Linda Kura,Piga Kura......Hakika Tunashinda!!!!

Monday, September 20, 2010

Mnyika azindua kampeni za Diwani kata ya Sinza Bw.Pamba Renatus Jumapili


Mnyika akimnadi Jukwaani Mgombea Udiwani Kata ya Sinza kupitia CHADEMA Bwana PAMBA Renatus jana viwanja vya Sevenup sinza palestina .

John Mnyika na Diwani wake wa Kata ya Sinza Pamba Renatus wakiomba Kura kwa wananchi wa Sinza Palestina jana

Mabere Marando naye alikuwepo kumnadi Mnyika na kuwasilisha ujumbe toka kwa Mgombea Uraisi kupitia CHADEMA Dr Slaa

Umatiulifika kusikiliza sera za Mnyika na Diwani wake. Nashukuru sana wale wote walioshiriki kuchangia safari ya Ushindi wa Jimbo la Ubungo katika mkutano ule wa Sinza kwa mkutano kuweza kukusanya Tsh laki moja na elfu sitini na mbili (162,000/-).

Saturday, September 18, 2010

Karibu Mikutano, 19.09.2010 Saranga/Kimara na Sinza

Ndugu,

Napenda kuwakaribisha mashabiki,wanachama,na wananchi wote katika mikutano yangu ya leo Jumapili,19.09.2010.Saranga/kimara na Sinza.

Saranga/Kimara; Mkutano wa ndani saa nne(4) asu mpaka saa sita(6) mchana(Thibitisha ushiriki;0715-393906/0755-393906).

Sinza,mkutano wa hadhara katika uwanja wa Seven Up eneo la Kumekucha kuanzia saa tisa(9) alasiri mpaka saa kumi na mbili(12)jioni. Tutazindua rasmi kampeni za mgombea Udiwani Kata ya Sinza, Ndugu Renatus Pamba.

Njoo ushiriki nasi katika safari hii ya ushindi-Wahimize na wengine unaowajua. Hakika Tunashinda!!


Daima; "Maslahi ya Umma Kwanza"!

Friday, September 17, 2010

Karibu mikutano ya ndani; Msigani/Mbezi na Makuburi 18.09.2010

Karibu kuunga mkono na kusikiliza sera; jumamosi 18.09.2010.
Mikutano ya ndani itafanyika katika kata ya Msigani/Mbezi kuanzia Saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana(wasilisha jina endapo unapenda kuhudhuria;0655-106368).

Makuburi saa 10 alasiri hadi saa 12jioni (wasilisha jina endapo unapenda kuhudhuria;0718-346811).

Njoo usikilize sera za kulibadili jimbo la Ubungo!
MASLAHI YA UMMA KWANZA.Mtaarifu mwenzako

"Kila la kheri Kaka MNYIKA uwe mbunge wetu"

Thursday, September 16, 2010

Mikutano yangu ya Kwembe,Kisopwa, Kiluvya na Msigani





Nikiwa na Mgombea Udiwani Kata ya Msigani

Wazee pia hujitokeza kwa wingi katika mikutano yangu. Hunihamasisha niendelee na harakati za kuletea maendeleo jimbo la Ubungo.

Miongoni wa makamanda akikusanya mchango wa mwananchi, michango ambayo huwa ni yahiyari kuwezesha kampeni zangu. Asanteni sana nyote mnaonichangia kuwezesha safari hii ya ukombozi wa jimbo la Ubungo.

Sehemu za fedha zilizokusanywa zikihesabiwa. Huwa tunatangaza kila mkutano kiasi tulichokipata papo hapo!

Peopleeee.........Powerrrrrr.......!!!!!!!!!!!!!!!!


Wednesday, September 15, 2010

Mkutano wa Mburahati

Baada ya kupita vichochoro na mitaa toka Magomeni Kagera hadi Mburahati, nilifanya mkutano wangu katika uwanja wa Mburahati pembeni kidogo mwa kituo cha Polisi.

Nashukuru wanahabari ambao mara kwa mara wamekuwa wakijitokeza katika mikutano yangu

Mgombea Udiwani Kata ya Manzese, Alhaji Kabunda akifanya mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Channel 5 "EATV"

Baada tu ya kumaliza mkutano wangu wa hadhara Mburahati niliweza kufanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha Channel 5 "EATV"

Tuesday, September 14, 2010

Mkutano wa Magomeni Kagera

Nikihutubia Mkutano wa Magomeni Kagera


Alhaji Kabunda akihutubia na kusisitiza jambo, pembeni yangu ni mgombea udiwani mwanamke pekee katika jimbo la Ubungo-Farida Momba.

Wakati mwingine tunahakiki nyaraka vizuri na kujadiliana. Ni kashfa za uuzaji wa viwanja vya wazi katika jimbo la Ubungo. Kashfa ambayo niliianika hadharani kupitia mkutano wa Magomeni Kagera

Kamanda Kotide akifanya vitu vyake kabla ya hotuba kuanza. Ni miongoni mwa hazina ya makamanda wenye karama ya uimbaji ndani ya CHADEMA.

Alhaji Kabunda, Mgombea Udiwani Kata ya Manzese

Umati wa Wananchi wa eneo la Magomeni-Kagera wakifatilia mkutano wangu.