Saturday, December 24, 2011

Heri ya Xmas, Tamasha la Injili na kutoa zawadi

Nachukua fursa hii kuwatakia heri katika sikukuu ya noeli. Kwa waumini siku hii ni kumbukumbu ya kwa mkombozi hivyo inapaswa kuleta mabadiliko ya kuzaliwa upya kiroho na kimaisha. Aidha nawahimiza kutumia siku hiyo kujumuika na waliokumbwa na matatizo mbalimbali katika jamii wakiwemo waathirika wa maafa ya maafuriko yaliyotokea Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yetu. Nawaalika kujumuika nami kwa hali na mali katika matukio ya tarehe 25 na 26 Disemba ambayo nitashiriki.

Katika kuadhimisha sikukuu ya mwaka huu pamoja na kujumuika na familia, tarehe 25 Disemba 2011 nitashiriki katika katika Tamasha la Muziki wa Injili na tarehe 26 nitatembelea nyumba za waathirika wa mafuriko eneo la Mabibo kutoa zawadi mbalimbali za sikikuu pamoja na kujumuika nao kwa chakula.

Katika kuadhimisha sikukuu hii nimealikwa kuwa Mgeni Rasmi katika tamasha la muziki wa Injili litakalofanyika katika Ukumbi wa Landmark Hotel-Ubungo siku ya Krismas kuanzia saa 8:30 mchana ambalo limeandaliwa na RudishaMusic ikishirikiana na WAPO Radio FM.

Lengo kuu la tamasha hili ni kusherehekea sikuku ya Noel-(Krismas) na kuendeleza jitihada za kukuza tasnia ya muziki wa Injili hapa nchini. Tamasha litahusisha vikundi mbalimbali vya muziki wa injli wa moja kwa moja (live performance) ambapo vikundi vitakavyoshiriki ni pamoja na Host of Praise, Glorious Celebration, Holy of Holies, Jackson Benty, Rachel Marlon na Mwanamapinduzi Band. (Maelezo zaidi kuhusu tamasha husika yanapatikana kupitia: www.XmasExtravaganza.co.tz.Katika kuadhimisha sikukuu ya kufungua zawadi (Boxing Day) tarehe 26 Disemba 2011 nitatembelea kaya mbalimbali za kata ya Mabibo ambazo zimeathiriwa kwa kiwango kikubwa na mafuriko kutoa zawadi mbalimbali za noeli na kula chakula cha mchana pamoja na waathirika wakubwa wa maafa. Nitatumia vile vile fursa hiyo kutoa ujumbe wangu wa kuwatakia wananchi wote wa Ubungo na watanzania kwa ujumla heri ya mwaka mpya 2012.

No comments: