Wednesday, February 29, 2012

Ratiba ya mbunge na DAWASCO kwenye kata leo, hatua zaidi zitafuata

Leo Machi Mosi nitakuwa pamoja na DAWASCO katika kata mbalimbali za jimbo la Ubungo kuchukua hatua za kuboresha upatikanaji wa maji kupitia ziara ya kikazi: Sinza (Saa 3-4 As), Mabibo/Makurumla (4-5), Makuburi (5-6), Saranga (6-7 mch), Msigani (7-8), Kwembe (8-9 jn).

Izingatiwe matatizo ya maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam ikiwemo katika Jimbo la Ubungo yamedumu kwa muda mrefu, tumepewa kazi ya kuwawakilisha kuisimamia serikali na mamlaka zake kupunguza kero husika katika kipindi cha muda mfupi; tunao wajibu wa pamoja wa kuziba pengo la miaka 50 katika kipindi cha chini ya miaka 5. Katika kipindi cha mwaka mmoja toka tupewe dhamana na dhima yapo maeneo ambayo tumewezesha yameanza kupewa mgawo wa maji, tuendelee kuunganisha nguvu ya umma zaidi katika mwaka huu wa pili wa 2012 yaongeze maeneo mengi zaidi.

Baada ya ziara hii tutawapa mrejesho kuhusu ratiba ya mgawo wa maji na hatua ambazo DAWASCO itapaswa kuendelea kuchukua. Nitawaeleza pia hatua za ziada ambazo tunapaswa kuchukua za kupanda ngazi kwenye mamlaka zingine hususan DAWASA, EWURA, Wizara ya Maji, Ofisi ya Rais na wadau wengine.

Tuendelee kushirikiana kila mmoja akichukua hatua kwa njia yake, maoni na ushauri pia unakaribishwa, wenye kutaka kuunganisha nguvu ya umma kupitia maandamano ya kuja kwa mbunge nao nawakaribisha; izingatiwe kuwa, maandamano yatayoratibiwa na ofisi ya mbunge kuwalenga wahusika wa juu zaidi yenyewe bado siku yake, tutafikia hatua hiyo iwapo serikali haitashughulikia kwa haraka masuala ambayo yanaweza kufanyika mwezi huu na kuonyesha kwa vitendo dhamira ya kutenga rasilimali za kutosha kwa mipango mingine inayoendelea kutekelezwa. Ni wakati wa mabadiliko ya kweli; tuwajibike. Maslahi ya Umma Kwanza, Twende Kazi.

3 comments:

Phiemon Kilibata said...

Tunakushukuru Mheshimiwa mbunge kwa kazi kubwa unayoifanya katika kutatua kero (matatizo ya wakazi wa Ubungo). Nimekuandikia mara kadhaa kuhusu tatizo la maji maeneo ya Kimara Baruti (Matete). Siku tuliyopata maji ya uhakika kwa mara ya mwisho ni tarehe 15 Januari, 2012. Naikumbuka sana siku hii kwa kuwa nilikuwa na harusi ya jirani yangu. Sisi tulioko Matete (karibu na kwa Mh. Koka) ambako ni juu sana ukilinganisha na Baruti hatupati maji kama yakiletwa katika kipindi ambacho watu wamekaa juma zima au zaidi. Naomba DAWASCO wafanye yafutayo:- Linapotokea tatizo tujulishwe kwa sms kama vile tunavyotumiwa bill; Maji yakifunguliwa watumishi wa DAWASCO wapite kila sehemu ili kujua kama maji yanafika; namba ya kutoa taarifa ya kukosekana maji, maji kuvuja itangazwe kama inavyotangazwa 112. Philemon kilibata 0713/0767/0783 310750 kilibata@iit-tz.com

Anonymous said...

Mh Mbunge hongera sana kwa jinsi unavyojitahidi kuwatumikia na kuwaunganisha wananchi wako wa jimbo la Ubungo. Kuna sehemu hapa sijawahi kuisikia ambayo pia wananchi wake wanateseka sana na hili tatizo la maji napo ni Golani, kijiweni. Eneo hili ambalo ukitokea suka unakumbana na huo mto ambao mvua kidogo tu ikinyesha haipitiki inahitaji daraja, maji ya mcihina yamepita lkn yanadivage kuelekea shule ya mringo iliyoko upande wa pili. Kwa hili unalizunngumziaje mheshimiwa mbunge

Hassan said...

Mh. Mnyika kweli tunaziona na kuzithamini juhudi zako na viongozi wenzako katika kutatua kero za Wananchi.

Hakika ziara ya jana yenye lengo la kujionea huduma ya maji katika jimbo lako ilikuwa chachu kubwa kwa DAWASCO, ofisi yako na Wananchi kwa ujumla.

Tumeona majukumu ambayo DAWASCO wanayopaswa kuyatekeleza, majukumu ya Serikali za Mitaa (Wananchi) na Viongozi wa kada mbalimbali za nchi.

Ni kweli kabisa kuwa changamoto za maji hazitaweza kwisha kama tukiwa tunaishia kulaumu tu. Tunapaswa kuoneshana njia ya kuyatatua kwa kutumia uwezo wetu wote tuliojaaliwa na Mungu.

Ushirikiano uliouonyesha uendelezwe kwani kila mmoja wetu ameshika ufito wa kujenga Dar es Salaam yenye huduma bora ya Maji. Kwani "baada ya Oksijeni hufuata Maji"

Kweli kwa pamoja tunaweza

Hassan
kemberajr@yahoo.co.uk