Friday, January 4, 2013

Washindi wa Shindano la Ujasiriamali Jimbo la Ubungo wapatikana

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa ushirikiano na shirika la Maendeleo Ubungo; Ubungo Development Initiative (UDI) waliendesha shindano la kuwainua wajasiriamali wadogo wadogo na hususan vijana wasio na ajira (na walio katika mazingira magumu) kwa kuwataka kuandaa mchanganuo namna gani watatumia Tsh 200,000/- katika kuanzisha au kuiendeleza biashara zao. Washindi waliopatikana ni;
Mshindi wa Kwanza: Joseph R. Shindo (22) kutoka Kata ya Kimara Tsh 200,000/-

Mshindi wa Pili: Rehema A. Abdallah (25) kutoka Makurumla Tsh. 100,000/-
Mshindi wa Tatu: Seif Juma (19) kutoka Goba Tsh 50,000/-
 
Washiriki wote wa shindano, pamoja na waratibu na Mbunge wa Jimbo la Ubungo

No comments: